KWA MUJIBU WA BIN ZUBERY
TIMU
ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku huu imefungwa mabao 2-1
kwenye Uwanja wa Marakech mjini hapa na wenyeji Morocco, Simba wa
Atlasi katika mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Kombe la Dunia Brazil mwakani.
Stars ilimaliza mechi hiyo pungufu baada ya Aggrey Morris kupewa kadi nyekundu dakika ya 37.
Hadi
mapumziko, Morocco walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na
Abderazak Hemed Allah baada yay eye mwenyewe kujiangusha kwenye eneo la
hatari baada ya kugongana na Aggrey Morris akatolewa nje.
Morocco ndiyo waliocheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza wakishambulia zaidi upande wa kulia alipokuwa akikimbiza Belhanda
Dakika ya 25 Thomas Ulimwengu alifanya kazi nzuri ya kumtoka beki, lakini shuti lake likadakwa na kipa.
Kocha
Kim Poulsen aliwapumzisha kwa mpigo washambuliaji Mrisho Ngassa na
Ulimwengu dakika ya 44 na kuwaingiza beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na
kiungo Khamis Mcha ‘Vialli’.
Kipindi
cha pili Morocco walirejea na moto tena, wakiishambulia zaidi Stars
iliyoonekana kudhoofika na katika dakika ya 50 Youssef El Arabi
akafunga bao la pili kiulaini baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania na
kubaki na kipa Juma Kaseja.
Hata
hivyo, shambulizi la kushitukiza liliipatia Stars bao la kufutia
machozi dakika ya 61 lililofungwa na Amri Kiemba kwa shuti la mbali
kutoka wingi ya kushoto.
Morocco
waliendelea kutawala mchezo na Stars walikuwa wakifanya mashambulizi ya
kushitukiza ambayo kwai kiasi fulani yalikuwa ya matumaini.
Dakika ya 82 Kim alimpumzisha Vialli na kumuingiza John Bocco ‘Adebayor’ ambaye aliongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
Kwa
matokeo hayo, Stars inabaki na pointi zake sita baada ya kucheza mechi
nne, kushinda mbili nyumbani na kufungwa mbili zote ugenini, nyingine
ikiwa dhidi ya Ivory Coast.
Lakini
Stars inabaki nafasi ya pili mbele ya Morocco yenye pointi tano sasa,
wakati Ivory Coast wanaongoza kwa pointi zao 10 baada ya kuifunga Gambia
3-0 leo.
Wiki
ijayo Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager watakuwa
wenyeji wa Ivory Coast mjini Dar es Salaam Morocco ikimenyana na Gambia.
Stars
inaweza kufufua matumaini ya kucheza Kombe la Dunia ikiifunga Ivory
Coast, kwani kama Tembo watafungwa na mechi ya mwisho na Tanzania
ikashinda, itasonga mbele.
Stars
inaondoka leo asubuhi hapa (juni 9) kwenda Casablanca kuunganisha ndege
kurejea Dar es Salaam ikipitia Cairo, Misri, tayari kuanza maandalizi
ya kuivaa Ivory Coast.
Katika
mchezo wa leo, kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Shomary Kapombe,
Erasto Nyoni, Kevin Yondan, Aggrey Morris, Frank Domayo, Amri Kiemba,
Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mchadk44/John Boccodk82, Mbwana
Samatta na Mrisho Ngassa/Nadir Haroub dk44.
No comments:
Post a Comment