Sunday, June 9, 2013

PATA UNDANI WA YALIYOTOKEA MECHI YA TAIFA STARS NA MOROCCO USIKU WA KUAMKIA LEO

KWA MUJIBU WA BIN ZUBERY
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku huu imefungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Marakech mjini hapa na wenyeji Morocco, Simba wa Atlasi katika mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani. 
Stars ilimaliza mechi hiyo pungufu baada ya Aggrey Morris kupewa kadi nyekundu dakika ya 37. 
Hadi mapumziko, Morocco walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Abderazak Hemed Allah baada yay eye mwenyewe kujiangusha kwenye eneo la hatari baada ya kugongana na Aggrey Morris akatolewa nje.
Morocco ndiyo waliocheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza wakishambulia zaidi upande wa kulia alipokuwa akikimbiza Belhanda
Dakika ya 25 Thomas Ulimwengu alifanya kazi nzuri ya kumtoka beki, lakini shuti lake likadakwa na kipa.   
Kocha Kim Poulsen aliwapumzisha kwa mpigo washambuliaji Mrisho Ngassa na Ulimwengu dakika ya 44 na kuwaingiza beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo Khamis Mcha ‘Vialli’. 
Kipindi cha pili Morocco walirejea na moto tena, wakiishambulia zaidi Stars iliyoonekana kudhoofika na katika dakika ya 50 Youssef El Arabi  akafunga  bao la pili kiulaini baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania na kubaki na kipa Juma Kaseja.  
Hata hivyo, shambulizi la kushitukiza liliipatia Stars bao la kufutia machozi dakika ya 61 lililofungwa na Amri Kiemba kwa shuti la mbali kutoka wingi ya kushoto.
Morocco waliendelea kutawala mchezo na Stars walikuwa wakifanya mashambulizi ya kushitukiza ambayo kwai kiasi fulani yalikuwa ya matumaini.
Dakika ya 82 Kim alimpumzisha Vialli na kumuingiza John Bocco ‘Adebayor’ ambaye aliongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.    
Kwa matokeo hayo, Stars inabaki na pointi zake sita baada ya kucheza mechi nne, kushinda mbili nyumbani na kufungwa mbili zote ugenini, nyingine ikiwa dhidi ya Ivory Coast.
Lakini Stars inabaki nafasi ya pili mbele ya Morocco yenye pointi tano sasa, wakati Ivory Coast wanaongoza kwa pointi zao 10 baada ya kuifunga Gambia 3-0 leo. 
Wiki ijayo Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager watakuwa wenyeji wa Ivory Coast mjini Dar es Salaam Morocco ikimenyana na Gambia.
Stars inaweza kufufua matumaini ya kucheza Kombe la Dunia ikiifunga Ivory Coast, kwani kama Tembo watafungwa na mechi ya mwisho na Tanzania ikashinda, itasonga mbele.
Stars inaondoka leo asubuhi hapa (juni 9) kwenda Casablanca kuunganisha ndege kurejea Dar es Salaam ikipitia Cairo, Misri, tayari kuanza maandalizi ya kuivaa Ivory Coast. 
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Kevin Yondan, Aggrey Morris, Frank Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mchadk44/John Boccodk82, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Nadir Haroub dk44.

HII INASHANGAZA LAKINI NI KWELI: ATEMBEA NA NYUMBA YAKE KWA MIAKA 5 AKIIBEBA. MCHEKI HAPA - BongoClan™ Website No1 Ya Vijana

HII INASHANGAZA LAKINI NI KWELI: ATEMBEA NA NYUMBA YAKE KWA MIAKA 5 AKIIBEBA. MCHEKI HAPA - BongoClan™ Website No1 Ya Vijana

Saturday, June 8, 2013

UNAJUA NANI KANG`AA KILI MUSIC AWARDS 2013!?

WALIOJINYAKULI TUZO MSIMU HUU.
kama bado hujajua nani kachukua tuzo msimu huu wa kili music awrd lile shindano kubwa la tuzo tanzania ni kama ifuatavyo hapa.
1. Mtunzi bora wa mashairi- Ben Pol.
2. Kundi bora - Jambo squard
3. Producer bora anayechipukia - Mensen Selectar
4. Msanii bora wa kiume - Diamond
5.Producer bora - Man Water
6. Msanii bora chipukizi - Aly Nipishe
7. Band Bora - (tuzo 3)- Charlz Baba
8. Bongo Pop- Ommy Dimpoz
9. Wimbo bora wa Zouk- Amini
10. Msanii bora wa kike - Rachel
11. Msanii bora wa Hiphop- Kala Jeremiah
12. Mtunzi bora wa mashairi ya hiphop- Kala Jeremiah
13. Wimbo bora wa Hiphop- Ney Wa Mitego
14. Wimbo bora wa RnB- Rama D
15. wimbo bora wa Africa Mashariki - Jose Chameleon (valuvalu0
16. Wimbo bora wa kushirikiana - Ommy Dimpoz & Vanessa Mdee (me & u)
17. Wimbo bora wa mwaka- Kala Jeremiah (Dear God)
18. Video bora ya mwaka- Ommy Dimpoz (baadae)
19. Msanii bora wa kike kiujumla- Lady Jay dee
20. Msanii bora wa kiume kiujumla - Diamond

UPANDE WA SHOO WALIJIPANGA KINOUMA NOUMA
Ilidondoshwa hiviii.......
Vijana kutoka Nyumba ya vipaji Tanzania (THT) Amini, Linnah, Ben Pol Pamoja na mkali Peter Msechu walidondosha bonge la burudani kwa wadau wa mziki waliohudhuria shughuli hiyo. pia wakali kama mzee Zahir Aly Zoro alifanya yake kinoumanouma na live band alipokamua kitu cha kikulacho cha Mr. Nice, ilibidi mashabiki wambandike manoti usoni jinsi mzee alivyokuwa mkali. snura hakuwa nyuma kushusha majanga hiyo jana. Vumilia naye alifanya yake kabla ya wakali mapacha watatu ku perform ile kinoumaaaaa!
Mkali mataluma pia alikuwepo, bila kumsahau Mwana FA. Mwisho THT dancers walishusha mautamu ya kufungia. kiufupi ilipendeza kiiinyama!
BARNABA
hakuna anayebisha kuwa huyu jamaa ni mkali, na mbunifu, alipanda kwa stage na bonge la gitar na kudondosha bonge la burudani.

GODZILLA KUMUENZI NGWAIR
Mashabiki walishindwa kuvumilia pale mkali wa ma freestyle aliyebakia Godzilla alipo muenzi mkali wa muda wote HAYATI ALBERT KENNETH MANGWAIR  kwa kupiga kitu cha Gheto langu, ilibidi mkali Mabeste na mwenzie Madee wavamie stage na kumuunga mkono Zilla kumuenzi mpendwa wetu Ngwair
 MFALME SELE
Mfalme wa mashairi anayedumu siku zote hakuacha kuwadondosha watu machozi pale alipokamua nyimbo special ya kumuenzi HAYATI ALBERT MANGWAIR.

Wednesday, June 5, 2013

R.I.P ALBERT KENNETH MANGWEAH

WATANZANIA WAKIUAGA MWILI WA NGWAIR KATIKA VIWANJA VYA LEADERS
 





JAMAA NA WAOMBOLEZAJI WENGINE WALIOPO MOROGORO
MAISHA YA MWANADAMU NI MAFUPI LAKINI KWA WALE WENYE UTU, URAFIKI, UPENDO NA UKARIMU KWA WENGINE HUISHI MAISHA MAREFU KATIKA MIOYO YA WAPENDWA WAO. ALBERT KENNETH MANGWEAH ATAKUMBUKWA DAIMA NA ATABAKI KATIKA MIOYO YA WATANZANIA DAIMA, SI KWA SABABU NI MWANAMZIKI MAARUFU ZAIDI KUWAHI KUISHI KATIKA TANZANIA, NBALI KWA USTAARABU WAKE NA UTULIVU WAKE. UPENDO WA KWELI NA UBORA WA KAZI YAKE YA MZIKI.
HAKUNA MTANZANIA ANAYE UJUA MZIKI NA ASIYE WEZA KUMFAHAMU MAREHEMU MANGWEAH, AMA NGWAIR KAMA ALIVYOJULIKANA KWA WENGI KUWA NI MKALI WA SIKU ZOTE WA STAILI HURU (FREESTYLES) NA ATABAKI KUWA HIVYO KAMA ALIVYOWAHI KUJINADI MWENYEWE KUWA "HATA NIKIFA SINA SPARE" NI KWELI HAKUTATOKEA SPARE YA KUZIBA PENGO LAKE.
WITO KWA WANAMZIKI WOTE KUIGA MEMA YOTE ALIYOKUWA AKIYATENDA MAREHEMU COWBAMA NA KUFANYA KAZI ZENYE VIWANGO NA UBORA WA HALI YA JUU ILI NAO PIA WAIGUSE MIOYO YA WATANZANIA KAMA ALIVYOFANYA STAR HUYO WA NGOMA KALI KAMA MSELA, CNN, GHETO LANGU NA ALBAMU NZIMA YA a.k.a MIMI ILIYOWAHI KUWA ALBAMU BORA YA MUZIKI TANZANIA KWA MUJIBU WA KURA ZA WATANZANIA NA KINYANG`ANYIRO CHA KILI MUSIC AWARDS.
POLE KWA NDUGU WA MAREHEMU, WANACHEMBA WOTE, MARAFIKI WA KARIBU, WANAMUZIKI WA TANZANIA NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA.
REST IN PEACE ALBERT KENNETH MANGAIR!!!!!!!!