WALIOJINYAKULI TUZO MSIMU HUU.
kama bado hujajua nani kachukua tuzo msimu huu wa kili music awrd lile shindano kubwa la tuzo tanzania ni kama ifuatavyo hapa.
1. Mtunzi bora wa mashairi- Ben Pol.
2. Kundi bora - Jambo squard
3. Producer bora anayechipukia - Mensen Selectar
4. Msanii bora wa kiume - Diamond
5.Producer bora - Man Water
6. Msanii bora chipukizi - Aly Nipishe
7. Band Bora - (tuzo 3)- Charlz Baba
8. Bongo Pop- Ommy Dimpoz
9. Wimbo bora wa Zouk- Amini
10. Msanii bora wa kike - Rachel
11. Msanii bora wa Hiphop- Kala Jeremiah
12. Mtunzi bora wa mashairi ya hiphop- Kala Jeremiah
13. Wimbo bora wa Hiphop- Ney Wa Mitego
14. Wimbo bora wa RnB- Rama D
15. wimbo bora wa Africa Mashariki - Jose Chameleon (valuvalu0
16. Wimbo bora wa kushirikiana - Ommy Dimpoz & Vanessa Mdee (me & u)
17. Wimbo bora wa mwaka- Kala Jeremiah (Dear God)
18. Video bora ya mwaka- Ommy Dimpoz (baadae)
19. Msanii bora wa kike kiujumla- Lady Jay dee
20. Msanii bora wa kiume kiujumla - Diamond
UPANDE WA SHOO WALIJIPANGA KINOUMA NOUMA
Ilidondoshwa hiviii.......
Vijana kutoka Nyumba ya vipaji Tanzania (THT) Amini, Linnah, Ben Pol Pamoja na mkali Peter Msechu walidondosha bonge la burudani kwa wadau wa mziki waliohudhuria shughuli hiyo. pia wakali kama mzee Zahir Aly Zoro alifanya yake kinoumanouma na live band alipokamua kitu cha kikulacho cha Mr. Nice, ilibidi mashabiki wambandike manoti usoni jinsi mzee alivyokuwa mkali. snura hakuwa nyuma kushusha majanga hiyo jana. Vumilia naye alifanya yake kabla ya wakali mapacha watatu ku perform ile kinoumaaaaa!
Mkali mataluma pia alikuwepo, bila kumsahau Mwana FA. Mwisho THT dancers walishusha mautamu ya kufungia. kiufupi ilipendeza kiiinyama!
BARNABA
hakuna anayebisha kuwa huyu jamaa ni mkali, na mbunifu, alipanda kwa stage na bonge la gitar na kudondosha bonge la burudani.
GODZILLA KUMUENZI NGWAIR
Mashabiki walishindwa kuvumilia pale mkali wa ma freestyle aliyebakia Godzilla alipo muenzi mkali wa muda wote HAYATI ALBERT KENNETH MANGWAIR kwa kupiga kitu cha Gheto langu, ilibidi mkali Mabeste na mwenzie Madee wavamie stage na kumuunga mkono Zilla kumuenzi mpendwa wetu Ngwair
MFALME SELE
Mfalme wa mashairi anayedumu siku zote hakuacha kuwadondosha watu machozi pale alipokamua nyimbo special ya kumuenzi HAYATI ALBERT MANGWAIR.